.

.

RADHA YA SHOW YA TIGO KIBOKO YAO

Tigo Kiboko yao ni show ya kivingine ambayo imefanyika katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo 25/1/2015, ikiwa ndio show kubwa iliyo fungulia mwaka wa 2015. Show ilikuwa na list ya wasanii wanao fanya poa katika Tasnia ambao walipanda jukwaani na kuwafanya mashabiki wao wapagawe kwa namna moja ama nyingine.
Mbali na kupata burudani ya kutosha kutokakwa wasanii wakubwa kama AY, Mwana FA, Ben Pol, Vanessa Mdee, Shaa, Linnah, Jux, Young D, Fid Q, Stamina, Young Killer Weusi, Professor Jay, Christian Bella Shilole, Yamoto Band nk, pia kulikuwa na burudani kubwa kwa wasanii ambao wadaiwa kupambanishwa katika show hiyo kwa kuangalia  ni nani mkali zaidi.
Ali Kiba na Diamond Platnumz: Show ya Alikiba ilikwenda poa kwa shangwe nyingi na show ilipendeza kuliko mfano shahidi mzuri ni yule aliyekuwepo kwenye tukio hilo, shangwe zilianza kusikika mara baada ya kukanyaga mguu wake kwenye stage hadi mwisho wa show, kelele za shangwe ndelemo na vifijo ndio zilizo tawala show yake. Na hata mara baada ya kumaliza show ilionekana wazi kuwa bado mashabiki wanamtaka aendelee na show, kwa sababu zisizo zuilika za muda alishuka stageni na kuwaacha mashabiki katika hali ya mzuka.
Pia kwa mpinzani wake Diamond Platnumz ambaye kwenye Fiesta alizomewa na mashabiki yeye katika show hii alipokelewa kwa shangwe nyingi pindi alipopanda kwenye stage, lakini ndani ya dakika kadhaa za mwanzo alirushiwa makopo kiasi kwamba kama angelikuwa ni msanii lege lege angepoteza muelekeo, lakini haikuwa hivyo kwa Diamond Platnumz bali aliamua kutumia Plan B yake na fikra za haraka kwa kujibu mashambulizi ya makopo kwa kuwarushia pesa mashabiki ndipo sekeseke la makopo likatuli shangwe, ndelemo na vifijo zikaendelea kama kawa hadi mwisho wa show yake.
Na hata mara baada show ya diamond kumalizika aliuliza kwa mashabiki wake “Tuendeleeeee” wakaitikia “tueendeleeeee” kwa sababu baadhi yao nadhani walikuwa wanataka ku- make kwa pesa ambazo Diamond alikuwa akiwarushia (Ahahaha mashabiki wa bongo bana ni shiida!!.)  Kifupi show ya wawili hao ilikuwa sawa na ilipendeza sana kwa sababu kila mmoja alitumia jitihada zake ili kuepukana na janga la kuzomewa Big up kwa wasanii na mashabiki wote walio jituma na kuonesha ushirikiano katika show hiyo. By Victor Petro



normal



bbbbbb







































- See more at: http://news.kutanisha.com/radha-ya-show-ya-tigo-kiboko-yao/#sthash.v8BkxF2X.dpuf
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: RADHA YA SHOW YA TIGO KIBOKO YAO Description: Rating: 5 Reviewed By: Anonymous
Scroll to Top